NYARAKA ZA ELIMU
1
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413, 2120403/4/
5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb.Na. TTDB/85/483/01/25
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM
Tarehe: 02/12/2009
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,
ZANZIBAR.
Katibu Mtendaji,
Baraza la Mitihani la Tanzania,
S.L.P. 2624,
DAR ES SALAAM.
KUH: MIHTASARI YA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA
STASHAHADA ILIYOREKEBISHWA NA UTARATIBU WA KUTAHINI
Rejea barua yenye Kumb. Na. TIE/MIN/ED/180/CA/IX/55 ya tarehe 3/9/2009
kuhusu shauri lililotajwa hapo juu.
Napenda kukuarifu kuwa tumepokea mihtasari ya aina nne (mipya na
iliyoboreshwa). Mihtasari iliyoboreshwa ni:
„X Mihtasari ya Ualimu ngazi ya Stashahada
„X Mihtasari ya Ualimu ngazi ya ChetiMihtasari miwili mipya ni:
„X Mihtasari ya Elimu kwa Michezo (Cheti)
„X Mihtasari ya Elimu ya Awali (Cheti)Malengo ya jumla ya Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada ni
kuandaa walimu wenye sifa walio na ujuzi na maarifa katika kufundisha Elimu ya
Msingi na ya Sekondari.
Mihtasari ya mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada ilikuwa inatekelezwa kwa
miaka 2: mwaka mmoja wa mafunzo chuoni na mwaka mmoja wa mazoezi ya
kufundisha shuleni. Aidha, mihtasari mipya ngazi ya cheti (kawaida) inafuta
2
matumizi ya mihtasari ya awali iliyokuwa inajumuisha masomo ya Maarifa ya
Jamii. Mihtasari ya Elimu kwa Michezo na ile ya Elimu ya Awali ni mipya.
Mihtasari yote minne ipo tayari kwa kutumika sasa kwa utaratibu wa mafunzo ya
miaka miwili chuoni. Mategemeo ni kwamba kupitia mafunzo ya ualimu wahitimu
watapata maarifa, ujuzi na stadi ili kumudu vema kazi ya kufundisha.
Utaratibu wa kutahini mihtasari ya stashahada ulikwisha tolewa kupitia barua
Kumb. Na. TTDB/193/437/OIA/6 ya tarehe 05/05/2008. Pamoja na ufafanuzi
kupitia barua Kumbukukumbu Na. TTDB/109/374/01/26 ya tarehe 6/7/2009.
Maelekezo ya kutahini yameweka mkazo katika: malengo, ujuzi maarifa stadi
muhimu, masomo ya kutahini, sifa zinazostahili kwa watahiniwa na viwango vya
utambuzi (‘distinction’, ‘credit’, ‘pass’ and ‘fail’). Kwa hiyo utahini wa mihtasari ya
ualimu ngazi ya cheti uzingatie misingi hii pia.
Sifa na muda wa mafunzo
Sifa ya chini ya kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi za Cheti (Cheti cha Ualimu,
Elimu ya Awali, Elimu kwa Michezo) bado itabaki ufaulu wa “Division IV” alama
28. Sifa za ziada za kujiunga na mafunzo ya ualimu Elimu ya Awali na
Elimu kwa Michezo zitaandaliwa na zitatolewa rasmi na kuanza kutumika mwezi
Julai, 2010.
Sifa kwa wale wanaojiunga na mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada kuanzia
tarehe 1 Julai 2009 ni “Principal pass” moja na “Subsidiary” moja katika masomo
yanayofundishwa shule za sekondari. Utaratibu huu ulikuwepo na utaendelea
mpaka itakapoelekezwa vinginevyo.
Sifa kwa wanaojiunga na mafunzo ya Stashahada ya Ualimu fani ya ufundi
itaendelea kuwa cheti cha FTC. Hata hivyo kwa lengo la kutoa fursa kwa
wahitimu wenye ufaulu mzuri katika masomo ya Sayansi na Hisabati, wasio na
cheti cha FTC wanaweza kujiunga na Stashahada ya Ualimu ya kawaida. Aidha,
kufuatia ‘phasing out’ ya programu ya FTC wenye sifa ya ‘NTA level 6’ na ambao
wangependa kusomea ualimu wanaweza kujiunga na ‘Diploma in Technical
Education’ wakati wale wa ‘NTAlevel 5’ watajiunga na Stashahada ya kawaida.
Utaratibu huu utatuwezesha kupata walimu wa fani hii na pia kutopoteza
wahitimu wenye ufaulu mzuri katika masomo ya Sayansi na Hisabati kwa ajili ya
shule za sekondari zenye mchepuo wa ufundi.
Muda wa mafunzo ya ualimu kwa programu zote (cheti cha ualimu, Elimu ya
Awali, Elimu kwa Michezo na Stashahada) utakuwa miaka 2.
3
Utambuzi na masharti ya kurudia
Kama ilivyopendekezwa awali, kwa mitihani ya ngazi zote za ualimu, ufaulu wa
kila mtahiniwa upimwe katika viwango vya madaraja manne (‘Distinction’,
‘Credit’, ‘Pass’ and ‘Fail’).
Katika ngazi ya Stashahada mtahiniwa atakayeshindwa masomo yasiyozidi nusu
ya masomo yote aliyotahiniwa katika mtihani ataruhusiwa kurudia. Mtahiniwa
atakayeshindwa masomo mawili ya kufundisha hataruhusiwa kurudia na atakuwa
ameshindwa. Vilevile mtahiniwa atakayeshindwa Mazoezi ya Kufundisha
hataruhusiwa kufanya mtihani na atakuwa ameshindwa. Mtahiniwa ataruhusiwa
kurudia masomo aliyoshindwa katika muda usiozidi miaka miwili tangu afanye
mtihani wa awali na fursa hii ni mara moja tu. Aidha anayerudia mitihani
anatakiwa afaulu masomo yote aliyorudia.
Mitihani ya mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti, Elimu kwa Michezo na Elimu ya
awali haitakuwa na utaratibu wa kurudia mitihani kwa wanachuo
watakaoshindwa mitihani mara ya kwanza.
Utahini wa Mafunzo ya Sayansi, TEHAMA na Lugha
Utaratibu wa kupima maendeleo ya kila siku ya mwanachuo uimarishwe, uwe na
uzito unaostahili na uwe wazi zaidi. Mafunzo kwa Vitendo (Practicals) kwamasomo ya Sayansi, TEHAMA na Lugha (English) yataimarishwa na
mwongozo utatolewa mara baada ya maandalizi kukamilika.
Pamoja na maelezo haya, utaratibu wa kutahini ulioandaliwa na kuanza kutumika
katika mihtasari ya stashahada ya mwaka 2009 uzingatiwe.
Kwa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti mabadiliko haya yana lengo la kuandaa
mwalimu anayemudu kufundisha masomo yote ya shule za msingi. Wanachuo
waandaliwe kufundisha masomo yote wakiwa mwaka wa kwanza. Watakuwa na
fursa ya kuchagua somo la ziada (option) wakiwa mwaka wa pili. Masomo ya
uchaguzi (options) yatatahiniwa pamoja na masomo ya lazima. Masomo ya
kuchagua ni pamoja na Vielelezo na Teknolojia, Commnication Skills, ICT na
Lugha za kigeni (mfano Kifaransa).
Pamoja na maelezo haya naambatanisha maelekezo kuhusu idadi ya mitihani
kwa kila ngazi ya mafunzo (Kiambatisho A). Aidha, orodha ya masomo ngazi ya
Stashahada, Cheti ngazi ya shule za Msingi, Elimu ya Awali na Elimu kwa
Michezo imeambatanishwa (Kiambatisho B).
4
Maelekezo haya yanaanza kutumika kuanzia tarehe 1 Julai 2009 na yatawahusuwanachuo walioanza mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti na stashahada mwezi
Julai 2009. Aidha, yatakuwa msingi wa kutahini kuanzia mitihani ya Mei 2011.
Nakutakia utekelezaji mzuri.
Umesainiwa na:
A. S. Mrutu
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala
1. Mkurugenzi, Taasisi ya Elimu Tanzania.
S. L. P. 35094
DAR ES SALAAM
2. Wakuu wa Vyuo vya Ualimu
TANZANIA BARA
3. Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
TANZANIA BARA
5
KIAMBATISHO A
Aina ya mafunzo ya Ualimu na mitihani yake, ujuzi stadi na maarifa ya kuzingatia katika kutahini.
Aina ya
mafunzo ya
Ualimu
Ujuzi, maarifa na stadi za kuzingatia Idadi ya mitihani na maeneo ya
kutahini
1. Elimu ya
Msingi
„X Ujuzi, unaoshirikisha wanafunzi kujifunza
„X Kuongoza wanafunzi wenye mahitaji tofautikatika kujifunza
„X Kuandaa na uwezo wa kutumia zana zakufundishia na kujifunza kwa usahihi
„X Uwezo na maarifa katika kushughulika namasuala mtambuka
„X Kujali na kuwasaidia wanafunzi wa shule zamsingi
„X Kuonyesha umahiri wa kufundisha masomoyafundishwayo shule msingi
„X Matumizi ya vielelezo na TEHAMA
„X Somo la Ualimu (mtihani 1)Masomo ya Taaluma
„X Masomo ya lazima: Geography,Historia, Uraia, Kiswahili, English,
TEHAMA, Haiba na Michezo,
Hisabati, Sayansi, na Stadi za Kazi.
* Masomo ya kuchagua
(chagua somo moja):
- Vielelezo na Teknolojia,Communication Skills, ICT, French
2. Elimu kwa
Michezo
„X Ujuzi unaoshirikisha wanafunzi kujifunzamichezo
„X Kuongoza wanafunzi wenye mahitaji tofautikatika kujifunza ngazi ya msingi
„X Kuandaa na kutumia zana za kufundishia nakujifunza michezo
„X Uwezo na maarifa katika kushughulika namaswala mtambuka
„X Kujali na kuwasaidia wanafunzi wa shule zamsingi kukuza vipaji katika michezo
„X Kuonyesha umahiri wa kufundisha michezoshule za msingi
„X Matumizi ya vielelezo na TEHAMA
„X Ualimu Michezo (mtihani 1 –lazima)
„X Masomo mawili ya Elimu kwaMichezo:
- Michezo (mtihani 1 lazima)
- Usimamizi na Usalama katika Michezo
(mtihani 1 – lazima)
„X Masomo ya lazima (Taaluma naUfundishaji – mtihani 1)
- Uraia
- Communication Skills
- Sayansi
6
- TEHAMA
- English
- Kiswahili
- Hisabati
* Masomo ya kuchagua: Chaguasomo moja kati ya: French au lugha
nyingine, ICT, Vielelezo na Teknolojia.
3. Elimu ya
Awali
„X Ujuzi wa kutumia njia zinazoshirikishawanafunzi kujifunza
„X Kujadili na kuwasaidia wanafunzi wa elimu yaAwali
Mitihani ya mwisho itakuwa na jumla ya
mitihani 10
(a) Somo la Ualimu (mtihani 1)
(b) Masomo ya Taaluma (lazima)
„X Communication skills (mtihani 1)
„X Uraia (mtihani 1)* Chagua somo moja kati ya:
„X Vielelezo na Teknolojia;
„X ICT( C) Vitendo vya kufundishia na
kujifunzia (vitendo 6)
„X Vitendo vya Hisabati (Taaluma +Ufundishaji)
„X Vitendo vya sanaa (Taaluma +Ufundishaji
„X Vitendo vya Kiswahili (Taaluma +Ufundishaji)
„X Vitendo vya Haiba na Michezo(Taaluma + Ufundishaji)
„X Vitendo vya Sayansi (Taaluma +Ufundishaji)
„X English Learning activities(Academic + Pedagogy)
7
KIAMBATISHO B
Orodha ya Mihtasari ya Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada
1. Education Psychology Guidance and Counselling
2. Currículum and Teaching
3. Foundation of Education
4. Education Research, Measurements and Evaluation
5. Education Media and Technology
6. Communication Skills
7. French Academic Syllabus
8. French Pedagogy syllabus
9. English Academic Syllabus
10. English Pedagogy syllabus
11. Muhtasari wa Utaalamu wa Kufundislha somo la Kiswahili
12. Muhtasari wa Taaluma wa somo la Kiswahili
13. Information and Communication Technology Syllabus
14. Information and Computer Studies
15. Physics Academic Syllabus
16. Chemistry Academic Syllabus
17. Chemistry Pedagogy Syllabus
18. Chemistry Pedagogy syllabus
19. Biology Academic Syllabus
20. Biology Pedagogy Syllabus
21. Mathematics Academic Syllabus
22. Mathematics Pedagogy Syllabus
23. Geography Academic Syllabus
24. Geography Pedagogy Syllabus
25. History Academic Syllabus
26. History Pedagogy Syllabus
27. Development Studies Syllabus
28. Civics Pedagogy Syllabus
Orodha ya Mihtasari ya Ualimu ngazi ya Cheti kwa Elimu ya Msingi, Michezo na Awali
A. Elimu ya Msingi
1. Ualimu Elimu ya msingi
2. Vielelezo na Teknolojia
3. Communication Skills
4. English
5. Kiswahili
6. French
7. Stadi za Kazi
8. Jiografia
9. Uraia
10. Historia
11. Sayansi
12. Hisabati
13. ICT
14. TEHAMA
15. Haiba na Michezo
8
B. Elimu kwa Michezo
1. Ualimu Michezo
2. Michezo
3. Usimamizi na Usalama katika Michezo
C. Elimu ya Awali
1. Ualimu Elimu ya Awali
2. Vitendo vya Masomo ya Elimu ya Awali
9
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb.Na. ED/OKE/NYK/2010/2
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM
Tarehe: 22 Februari, 2010
Makatibu Tawala wa Mikoa,
Makatibu Tawala Wilaya,
Wakurungenzi; Halmashauri za Miji/Manispaa/Jiji,
Wakurugenzi Watendaji; Halmashauri za Wilaya,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya,
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi,
TANZANIA BARA.
WARAKA WA ELIMU NA. 2 WA MWAKA 2010
VITABU VYA KIADA SHULENI
Mwaka 1991 Wizara ya Elimu na Utamaduni ilitoa sera kuhusu upatikanaji na
usambazaji wa vitabu shuleni na vyuoni. Sera hii ambayo ilianza kutumika tarehe
1 Januari 1992 inahalalisha mfumo wa matumizi ya kitabu zaidi ya kimoja cha
kiada katika shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu ili mradi vitabu hivyo
viwe vimepata ithibati. Utaratibu huu hauweki ukomo au madaraja ya ubora wa
vitabu vilivopata ithibati. Hali hii imesababisha kuwepo kwa vitabu vingi vya kiada
vilivyopata ithibati kushindania soko.
Wizara imebaini kuwa kutokana na hali hii shule zinajikuta zikitumia vitabu vya
kiada tofauti. Aidha, kwa kuwa uwezo wetu wa kununua vitabu shuleni ni mdogo,
imebidi shule nyingi zichague kitabu kimoja au viwili kama vitabu vya kiada bila
kuwa na fursa ya kuona vitabu vyote vilivyopewa ithibati katika masomo husika ili
ziweze kufanya uchaguzi muafaka. Kwa maana hiyo, wanafunzi walikosa fursa
sawa ya kupata maarifa kutoka katika chaguo pana la vitabu vilivyopewa ithibati
na hatimaye kusababisha kukosekana kwa ulinganifu wa ubora wa ufundishaji na
ujifunzaji.
10
Kufuatia hali hii, Wizara inapitia upya utaratibu huo wa matumizi ya kitabu zaidi
ya kimoja cha kiada kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwa mabadiliko hayo
hayataleta athari katika utoaji wa elimu nchini.
Wakati utaratibu huo unapitiwa, Wizara imeamua kwamba kila Somo na kila
Darasa husika litakuwa na vitabu viwili teule vya kiada ili kuhakikisha kwamba
vitabu vya kutosha vinapatikana shuleni. Vitabu vya kiada vilivyochaguliwa kwa
sasa ni vile vya ngazi ya Elimu ya Awali na ngazi ya Elimu ya Msingi kwa Darasa
la Kwanza hadi laTano.
Orodha ya vitabu hivyo imeambatishwa na Waraka huu. Vitabu vya Darasa la
Sita na la Saba havitahusika kwa sasa, hivyo utaratibu uliokuwepo utaendelea
kutumika. Aidha, vitabu vyote vyenye ithibati ambavyo havikuchaguliwa kutumika
kama vya kiada vitatumika kama vitabu vya rejea na ziada katika kujifuna na
kufundishia.
Utaratibu wa kuteua vitabu vya kiada kwa Darasa la Sita na la Saba na kwa
ngazi ya Sekondari na Vyuo vya Ualimu unaandaliwa.
Wizara inaomba ushirikiano kutoka kwa wadau wote katika kutekeleza
mabadiliko hayo.
Waraka huu unaanza kutumika mara moja.
Umesainiwa na:
A. S. Mrutu
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
11
Kiambatisho A.
VITABU VILIVYOPENDEKEZWA
12
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR
ES SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. ED/OKE/NYE/VOL. 1/01
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 28/04/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
Maafisa Elimu wa Msingi wa Wilaya
TANZANIA BARA
WARAKA WA ELIMU NA. 1 WA MWAKA 2011
MASOMO YATAKAYOTAHINIWA KATIKA MTIHANI WA KUHITIMU ELIMU
YA MSINGI
Masomo yanayofundishwa katika Elimu ya Msingi ni Hisabati, Kiswahili, English,
Sayansi, Historia, Jiografia, Stadi za Kazi, TEHAMA, Uraia, Haiba na Michezo,
Kifaransa na Dini. Kati ya masomo hayo, masomo ya lazima ni Hisabati,
Kiswahili, English, Sayansi, Historia, Jiografia, Dini, Uraia, Stadi za Kazi, Haiba
na Michezo.
Aidha, masomo ya Kifaransa TEHAMA na Dini ni ya ziada (optional). Kutokana
na umri na uwezo wa kujifunza wa mwanafunzi wa shule ya msingi, masomo
haya ni mengi kwake kuyamudu na kuyafanyia mtihani.
Kwa msingi huo, Wizara iliamua kuwa masomo yatakayotahiniwa katika mtihani
wa kuhitimu Elimu ya Msingi ni Hisabati, Kiswahili, English, Sayansi na Maarifa
(Historia, Jiografia na Uraia) na yatatahiniwa kwa muda wa siku mbili mfululizo.
Msimamo wa Wizara ni kuendelea kutahini masomo hayo. Masomo mengine
yatafundishwa kikamilifu bila kutahiniwa.
Waraka huu unaanza kutumika mara moja
13
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
1. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
2. Wakurugenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
14
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR
ES SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb.Na. ED/OKE/NYE/VOL.1/02
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 29/04/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
Maafisa Elimu Msingi/Sekondari wa Wilaya
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu
Wakuu wa Shule za Sekondari
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi
TANZANIA BARA
WARAKA WA ELIMU NA. 2 WA MWAKA 2011
TARATIBU ZA UANDIKISHAJI WANAFUNZI/WANACHUO KWA KUZINGATIA
URAIA
Imebainika kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wanaoandikishwa katika shule za
serikali na zisizo za serikali bila kubainishwa uraia wao na hivyo kusababisha
watu hao kusoma na kuajiriwa kama raia wa Tanzania baada ya kuhitimu
masomo/kozi zao. Hali hii imesababishwa na uandikishaji wa wanafunzi
usiozingatia kipengele cha uraia wao.
Kutokana na hali hiyo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaagiza
kuzingatiwa kwa taratibu za uandikishaji wa wanafunzi katika ngazi zote za elimu
kwa kuzingatia kipengele cha uraia wa wanafunzi. Kwa hiyo kila mwanafunzi
anayeandikishwa ni lazima aoneshe cheti cha kuzaliwa au uthibitisho wa uraiawake.
Utaratibu huu utasaidia kutambua uraia wa wanafunzi na wanachuo.
Waraka huu unaanza kutumika Januari, mwaka 2012.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
15
Nakala:
1. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
2. Wizara ya Mambo ya Ndani
3. Wakurungenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
4. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
16
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na ED/OKE/NYE/VOL.1/03
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 29/04/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
Maafisa Elimu wa Msingi/Sekondari wa Wilaya
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu
Wakuu wa Shule za Sekondari
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi
TANZANIA BARA
WARAKA WA ELIMU NA. 3 WA MWAKA 2011
KUZOROTA KWA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU KWA WALIMU NA
WANAFUNZI
Kusoma vitabu na makala mbalimbali ni mojawapo ya njia ya kupata maarifa kwa
mtu yeyote. Kujisomea vitabu ni njia muhimu sana kwa walimu na wanafunzi ili
kukuza stadi ya kufundishia na kujifunzia.
Utamaduni huu wa kujisomea vitabu na makala mbalimbali miongoni mwa
walimu na wanafunzi umekuwa ukizorota siku hadi siku. Hali hii, imesababisha
baadhi ya walimu kushindwa kufundisha ipasavyo na wanafunzi kuwa tegemezi
kwa maarifa yanayotolewa na walimu wao. Ikumbukwe kwamba ili wanafunzi
waweze kujifunza vizuri, wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima
wa kujifunza ikiwa ni pamoja na kuibua na kutetea hoja zao.
Madhumuni ya waraka huu, ni kusisitiza kufufua utamaduni wa kujisomea vitabu
na makala mbalimbali kwa walimu na wanafunzi ili kuboresha mawanda ya
ufundishaji na ujifunzaji.
Kwa kuzingatia mazingira ya shule husika, kila mkuu wa shule/mwalimu mkuu
ahakikishe wanafunzi na walimu wanajenga tabia ya kujisomea vitabu na makala
mbalimbali.
17
Kwa waraka huu inaagizwa kuwa, maktaba za shule zifufuliwe na pale ambapo
hazikuwepo zianzishwe.
Waraka huu unaanza kutumika Januari, 2012
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
1. Katibu Mkuu, ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
2. Wakurugenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
18
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. ED/OKE/NYE/VOL.1/04
S. L. P. 9121
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 28/04/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
Maafisa Elimu wa Msingi/Sekondari wa Wilaya
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu,
Wakuu wa Shule za Sekondari
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi
TANZANIA BARA.
WARAKA WA ELIMU NA. 4. WA MWAKA 2011
KUDHIBITI JANGA LA MOTO KATIKA SHULE NA VYUO VYA UALIMU
NCHINI
Siku za hivi karibuni janga la moto limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika
shule. Janga hili limesababisha maafa na hasara kubwa kwa serikali na jamii
ikiwemo kupoteza mali na maisha ya wanafunzi.
Wizara imechunguza sababu za kuwepo kwa janga la moto na kubaini kuwa
baadhi ya shule huendeshwa bila kuzingatia mambo muhimu ya kudhibiti janga
hili la moto. Kujihami na janga hili ni suala linalohitaji kuweka mikakati thabiti ya
kupambana na janga hili. Katika kudhibiti janga hili la moto, Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, inawahimiza wadau wa elimu hususan walimu wakuu wa
shule za Msingi, Wakuu wa shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu kuhakikisha
kuwa asasi zote za elimu zinatekeleza mambo yafuatayo:
„h Kuwa na vifaa vya kuzimia moto na vihisi moshi (smoke detectors)vinavyofanya kazi na vinakaguliwa mara kwa mara;
„h Kuwa na mifumo ya nyaya za umeme iliyo madhubuti na inayokaguliwamara kwa mara;
„h Kuwepo kwa milango ya dharura inayofunguka kwa nje katika majengoyote yanayokusanya watu pamoja mfano, mabweni, maabara na bwalo la
chakula/mikutano;
19
„h Kila asasi ipige marufuku matumizi ya vibatari na mishumaa ndani yamabweni/daharia;
„h Kuhakikisha kuwa hakuna msongomano wa wanafunzi katikamabweni/daharia;
„h Kuwapatia wanafunzi elimu ya tahadhari ya milipuko ya moto na majangamengine; na
„h Kuhakikisha kuwa wanafunzi hawapiki wala kupiga pasi ndani yamabweni/daharia kwa kutumia pasi za mkaa na umeme, kitengwe chumba
maalum kwa ajili ya kupigia pasi.
Maafisa Elimu wa Halmashauri wanashauriwa kufuatilia utekelezaji wa suala hili
katika Halmalshauri zao.
Waraka huu unaanza kutumika Januari, 2012
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
1. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
2. Wakurugenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
20
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na.ED/OKE/NYE/VOL.1/05
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 28/04/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
Maafisa Elimu wa Msingi/Sekondari wa Wilaya
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu,
Wakuu wa Shule za Sekondari
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi
TANZANIA BARA.
WARAKA WA ELIMU NA. 5 WA MWAKA 2011
UTARATIBU WA KUWASIMAMISHA/KUWAFUKUZA SHULE WANAFUNZI
WATORO KATIKA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU
Pamekuwepo na ukiukwaji wa kanuni na taratibu za kushughulikia kesi za
wanafunzi watoro shuleni/vyuoni. Baadhi ya walimu wakuu na wakuu wa
shule/vyuo wamekuwa na utaratibu usiozingatia maelekezo kuhusu uendeshaji
wa shule/vyuo kama zilivyoanishwa kwenye kiongozi cha mwalimu mkuu na
mkuu wa shule/chuo kwa kujichukulia hatua mkononi kwa kuwasimamisha na
kuwafukuza wanafunzi hao. Hali hii imesababisha kuwepo kwa malalamiko
miongoni mwa wanajamii, na kama itaachwa iendelee itasababisha usumbufu
mkubwa kwa pande zinazohusika.
Kutokana na hali hiyo, wizara imelazimika kutoa waraka kukemea tabia hii.
Kuanzia sasa ni marufuku kwa mwalimu mkuu au mkuu wa shule/chuo
kumsimamisha/kumfukuza shule mwanafunzi mtoro bila kuzingatia taratibu
zilizowekwa. Kama mwanafunzi hatafika shuleni/chuoni kwa muda wa siku 30
mfululizo bila kutoa taarifa kwa uongozi wa shule/chuo atasimamishwa masomo,
na kama ataendelea kuwa mtoro hadi kutimia siku 90 mfululizo atafukuzwashule na kikao halali cha kamati / bodi ya shule/chuo.
21
Kwa upande wa makosa mengine ya kinidhamu kanuni na taratibu zilizoanishwa
kwenye kiongozi cha mwalimu mkuu na mkuu wa shule/chuo zitaendelea
kutumika.
Waraka huu unaanza kutumika mara moja.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
1. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
2. Wakurugenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
22
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. ED/OKE/NYE/VOL.1/06
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 27/04/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
Wakuu wa Shule za Sekondari/Vyuo
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi
TANZANIA BARA.
WARAKA WA ELIMU NA. 6 WA MWAKA 2011
KUPIGA MARUFUKU UTITIRI WA MITIHANI
Mtihani ni njia inayotumiwa kumwezesha mwalimu kujua kiwango cha uelewa wa
wanafunzi kuhusu mada zilizofundishwa kwa kipindi fulani.
Kumezuka mtindo wa baadhi ya walimu kutunga mitihani mbalimbali na
kuwapatia wanafunzi bila kuzingatia madhumuni ya mitihani katika mchakato
mzima wa kujifunza. Walimu hao wanatunga mitihani na kuwapa wanafunzi
wafanye kwa kulipia fedha kitendo hicho ni kinyume na taratibu na maadili ya
ufundishaji.
Aidha, mitihani hii hufanyika kila mara kitendo kinachopunguza muda mwingi wa
ufundishaji, mitihani hiyo ni kama: `speed test’, Mitihani ya Wiki, Mitihani ya
Ujirani Mwema na Mitihani ya Mwezi. Mitihani yote hii wanafunzi huchanga
fedha.
Ili kupunguza utitiri wa mitihani, Wizara inashauri mitihani ifuatayo ndio itiliwe
mkazo.
„h Mitihani ya Nusu Muhula
„h Mitihani ya Muhula
„h Mitihani ya MweziAidha, mitihani hii ifanyike bila kuchangisha fedha wanafunzi.
23
Kwa Waraka huu ninaagiza kuacha mara moja kuwapa wanafunzi mitihani
inayotolewa bila lengo maalumu. Mazoezi ya darasani yatumike kupima uelewa
wa mada zilizofundishwa.
Mwalimu yeyote atakayebainika akichangisha fedha kwa kisingizio cha
kugharimia mitihani atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Waraka huu unaanza kutumika mara moja.M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
1. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
2. Wakurugenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
24
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. ED/OKE/NYE/VOL.1/07
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 29/04/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu
Wakuu wa Shule za Sekondari
Walimu Wakuu wa Shule za Awali/Msingi
TANZANIA BARA
WARAKA WA ELIMU NA. 7 WA MWAKA 2011
UBORESHAJI WA ELIMU YA MAZINGIRA YA SHULE/VYUO
Mazingira ni vitu vyote vinavyoizunguka jamii.
Mazingira mazuri shuleni huleta uelewa wa haraka kwa mwanafunzi na motisha
kwa mwalimu katika ujifunzaji na ufundishaji kwa kutumia mifano halisi iliyo
katika mazingira ya shule. Hivyo, mazingira mazuri ni kivutio kwa shule na jamii.
Ili kuhifadhi mazingira na kuleta mandhari nzuri ya shule vitu kama usafi,
michezo mbalimbali, bendi ya shule na gwaride vinaongeza mvuto.
Wizara inawakumbusha Maafisa Elimu wote, Wakuu wa Shule za Msingi,
Sekondari na Vyuo vya Ualimu kuhimiza utekezaji wa yafuatayo:-
„h Kupanda miti (miti ya kivuli, matunda, mbao na kuni)
„h Kupanda maua
„h Kupanda ukoka/nyasi
„h Kupanda ‘hedges’ pembeni mwa barabara zote za shule
„h Kupanda mawe na kuyapaka chokaa
„h Kuweka mipaka thabiti ya shule
„h Kuboresha na kuanzisha miradi mbalimbali
„h Kutengeneza viwanja, kufufua na kudumisha michezo mbalimbali
„h Kufufua na kudumisha bendi za shule
„h Kutayarisha ramani za: -
25
(a) Wilaya yao katika eneo la shule kwa kutumia vifaa vinavyopatikana
kwa urahisi katika mazingira yao
(b) Mkoa wao
(c) Tanzania
(d) Afrika
(e) Dunia
„h Kuingiza dhana za Elimu ya Mazingira katika masomo yoteyanayofundishwa shuleni.
„h Kuingiza dhana za Elimu kwa Maendeleo Endelevu katika masomo yoteyanayofundishwa shuleni.
„h Kutumia vyombo/vifaa vya kisayansi kufanya utafiti katika mazingira.
„h Kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, Siku ya Kunawa Mikono Duniani,n. k.
„h Kutupa taka zikiwa zimechambuliwa katika sehemu maalum (takazinazooza, taka zisizooza, plastiki, maji machafu, chupa, n. k.)
„h Kuhakikisha kuwa chakula kinatunzwa katika sehemu safi na zisizoruhusuwadudu na sumu kufikia chakula hicho.
Waraka huu unarekebisha Waraka Na. 11 wa mwaka 1998 na unaanza
kutumika mara moja.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
1. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
2. Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais
3. Wakurugenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
26
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. ED/OKE/NYE/VOL.1/08
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe : 29/04/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa,
Makatibu Tawala wa Wilaya,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya,
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu,
Wakuu wa Shule za Sekondari,
Walimu Wakuu wa Shule za Awali/Msingi,
TANZANIA BARA.
WARAKA WA ELIMU NA. 8 WA MWAKA 2011
KUKITHIRI KWA MICHANGO SHULENI
Wizara ilitoa Waraka wa Elimu Namba 2 wa Mwaka 1999 wenye Kumb. Na.
ED/OK/C.2/4/50 uliohusu michango ya kuendeleza shule.
Tangu kipindi hicho hadi sasa imebainika kwamba, baadhi ya shule zisizo za
serikali na hata za serikali zimekuwa zikiendelea kutoza wazazi michango
kiholela hata pale isipostahili na bila kibali cha wizara au Kamati za shule, Bodi
za shule na Halmashauri husika. Michango hii imekuwa ni kero kubwa kwa
wazazi na wanafunzi na hata kusababisha baadhi ya wanafunzi kuacha shule na
wengine kuwa watoro.
Aidha, baadhi ya michango inayodaiwa ni ya kununulia vifaa vya kujifunzia na
kufundishia kujenga majengo na samani. Baadhi ya shule hutoza michango ya
majengo kila mwaka, ingawa majengo hayo hayaendelei kujengwa au vifaa na
samani hizo haziongezeki badala yake upungufu wa vitu hivyo huendelea
kuwepo shuleni. Pia kutoza michango mbalimbali ya mitihani isiyo na idadi.
Uwingi wa michango isiyoratibiwa ni kinyume cha taratibu na inaongeza mzigo
kwa wazazi na kusababisha wanafunzi kukosa masomo pale wanapofukuzwa
kwa kutolipa michango hiyo.
27
Kwa Waraka huu, Wizara inaagizwa kuwa Michango yote ya maendeleo ya shule
idhibitiwe kwanza na Wanajamii wote, Kamati ya Shule/Chuo, Bodi yaShule/Chuo na Halmashauri husika. Aidha, utaratibu wa kukusanya michangohiyo usihusishe wanafunzi.
Shule yoyote ambayo itahitaji kuchangisha wazazi michango, ni sharti wazo hilo
lijadiliwe na Kamati/Bodi ya shule na wazazi washirikishwe kwenye kikao cha
walimu ili maoni yatolewe.
Maombi ya kuchangisha michango ni budi yatumwe kwenye Halmashauri husika
ambapo kibali kitatolewa au kukataliwa. Michango yote iliyokubaliwa
kuchangishwa itatolewa na wanajamii au wazazi na sio wanafunzi. Jukumu la
kukusanya michango litabaki mikononi mwa wanajamii, hivyo jamii iandae
taratibu zao za kuhakikisha michango waliyopitisha wenyewe inachangishwa bila
kuwabughudhi wanafunzi.
Aidha, kwa shule zisizo za serikali zisitoze wanafunzi michango ya aina yoyote
ya maendeleo ya shule kwani shule binafsi ni rasilimali ya mwenye shule.
Michango ambayo ni kero ni kama ifuatavyo:
„h Michango ya kuandikisha wanafunzi Darasa la Kwanza/Kidato chaKwanza.
„h Barua za utambulisho wa wanafunzi wanaofaulu Darasa la Saba kwendashule za sekondari.
„h Barua zote za wanafunzi kuitwa kujiunga na shule za sekondari / vyuo.
„h Fomu za kujiunga na Kidato cha Kwanza katika shule zisizo za serikali.Inaagizwa kuwa barua zote za kuitwa kujiunga na shule zipitiwe na kupata kibali
cha Mkaguzi Mkuu wa Shule wa Wilaya/ Kanda husika baada ya kuridhika kuwa
michango inayoagizwa imepata kibali cha Halmashauri husika.
Waraka huu unafuta nyaraka zote za nyuma zinazohusu michango ya
kuendeleza shule na unaanza kutumika mara moja.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
28
Nakala:
1. Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania
2. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI
3. Wakurugenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
29
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413, 2120403/4/
5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. ED/OKE/NYE/VOL.1/10
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 29/04/2011
Makatibu Tawala Mikoa,
Makatibu Tawala Wilaya,
Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania,
Wakaguzi Wakuu wa Shule (K),
Maafisaelimu wa Mikoa,
Maafisaelimu wa Wilaya, Msingi na Sekondari,
Wakaguzi Wakuu wa Shule (W),
Wakuu wa Shule za Sekondari zisizo za Serikali,
Walimu Wakuu wa shule za Msingi zisizo za Serikali,
TANZANIA BARA.
WARAKA WA ELIMU NA. 10 WA MWAKA 2011
MASHARTI MAPYA YA USAJILI WA SHULE
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ndiyo msimamizi wa Elimu nchini kwa
mujibu wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 na sheria ya Elimu Na.25
ya Mwaka 1978 na rekebisho lake Na. 10 la Mwaka 1995.
Kuanzia mwanzoni mwa mwaka 1980 serikali iliruhusu wadau mbalimbali
wakiwemo watu binafsi na Taasisi zisizo za Serikali kutoa elimu katika ngazi
mbalimbali za elimu hapa nchini zikiwemo:- Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na
Vyuo vya Mafunzo ya Ualimu
Serikali inapongeza juhudi za wadau mbalimbali mathalan mashirika ya dini,
taasisi mbalimbali, watu binafsi na Halmashauri kwa kuitika wito huo.
Hata hivyo, mashirika, taasisi mbalimbali na watu binafsi wenye uwezo wa
kuanzisha shule zisizo za serikali hapa nchini, wanashauriwa kuzingatia masharti
yaliyoainishwa katika sheria na miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara.
Mwenye nia na uwezo wa kuanzisha Shule/Chuo cha ualimu ni lazima atimize
masharti yafuatayo:-
30
„h Awe na eneo lisilopungua Hekta 3 kwa maeneo ya vijijini na 1.5 kwa eneola mjini lililotolewa kwa madhumuni ya Elimu na Mamlaka husika (Wizara
ya Ardhi na Serikali za vijiji).
„h Aombe kibali cha kujenga majengo ya shule/chuo kwa kufuata ramanizilizopendekezwa na Wizara ama zitakazokubaliwa na Wizara na ambazo
zimepitishwa na mamlaka za Halmashauri husika (Mhandisi wa Wilaya na
Mipango Miji wa Wilaya).
„h Akamilishe majengo muhimu ya mwanzo yakiwemo madarasa yakutosheleza wanafunzi wa mwaka wa I na II, jengo la utawala/ofisi za
walimu, bwalo/ukumbi, maabara moja kwa kuanzia, maktaba, vyoo vya
wasichana, wavulana na wafanyakazi na samani.
„h Aombe kuthibitishwa kuwa Mwenye Shule/chuo na Meneja wa Shule kwakujaza fomu Na. RS 6 na RS 7 na kuziwasilisha kwa Afisa Elimu wa
Wilaya/Mji/Manispaa ilipojengwa shule kwa maoni na mapendekezo. Pia
Mwenye Shule/chuo mtarajiwa atatakiwa kuwaomba Maafisa wa Afya,
Mhandisi wa Majengo na Mkaguzi Mkuu wa Shule (wote wa Wilaya)
Mji/Manispaa wafanye ukaguzi na taarifa zao zitatumiwa kuona hali halisi
na utayari wa majengo na mazingira ya shule/chuo.
Baada ya Mwenye Shule/Chuo na Meneja kuthibitishwa atajaza fomu na. RS. 8
ya kuomba kusajili Shule/Chuo. Fomu hii itawasilishwa kwa Mkaguzi Mkuu wa
Shule wa Kanda shule ilipojengwa. Endapo shule ina sifa stahili itasajiliwa nakupewa namba ya usajili na ndipo itaruhusiwa kuandikisha wanafunzi.
Tendo la kusajili litakuwa endelevu, na litajirudia kila baada ya miaka minne (4) ili
kuhakikisha kwamba viwango vilivyowekwa vinazingatiwa.
Shule/Chuo kitasajiliwa iwapo kitakuwa kimetimiza masharti yote ya usajili na
kupewa namba ya mtihani.
Waraka huu unafuta nyaraka zote za nyuma na unaanza kutumika kuanzia
Januari, 2012.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
1. Katibu Mkuu, Ofisi ya waziri Mkuu TAMISEMI
2. Wakurugenzi wote , Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
31
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. ED/OKE/NYE/VOL.1/11
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe 29/04/2011
Makatibu Tawala Mikoa,
Makatibu Tawala Wilaya,
Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Wilaya/Miji/Manispaa/Jiji
Wakaguzi Wakuu wa Shule (K),
Wakaguzi Wakuu wa Shule (W),
Wakuu wa Shule za Sekondari,
Walimu wakuu shule za Msingi,
TANZANIA BARA.
WARAKA WA ELIMU NA. 11 WA MWAKA 2011
UENDESHAJI WA MITIHANI YA KUMALIZA NGAZI MBALIMBALI ZA ELIMU
KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU
Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wamekuwa wakijumuishwa kwa muda wote
wa kujifunza darasani. Kwa mujibu wa Waraka huu, wanafunzi wenye ulemavu
wanaolengwa ni wale ambao ulemavu wao umethibitishwa na mamlaka kuanzia
shule hadi wizara kuwa wanahitaji huduma inayokusudiwa.
Yamekuwepo malalamiko toka kwa wazazi wa wanafunzi wenye ulemavu kuwa
waendesha mitihani hawazingatii mahitaji ya kundi hili la watahiniwa.
Ili kuwawezesha kufanya mitihani kama wanafunzi wenzao maandalizi ya
mitihani, ufanyaji wake na usahihishaji lazima utambue mahitaji maalumu
waliyonayo wanafunzi wenye ulemavu.
Mahitaji hayo yapo katika maeneo yafuatayo:
„h Wasioona hutumia muda mwingi kuchomoa na kupachika karatasi kwenyemashine ya kuandikia.
„h Wenye ulemavu wa viungo hupata shida ya kuandika (kitetemeshi) auwaendapo kujisaidia hutumia muda mrefu kurudi katika chumba cha mtihani
na wengine kuandika kutumia miguu au kichwa.
32
„h Wenye ulemavu wa akili kufikiri polepole hadi kupata kitu cha kuandika.Waanzapo kuandika kasi yao ya kuandika ni ndogo.
„h Wenye uoni hafifu (wakiwemo Albino) husoma kwa shida maandishi yakawaida, hivyo kuhitaji maandishi yaliyokuzwa.
„h Viziwi hupata shida ya kutafsiri lugha ya kawaida kwa kuitenganisha nalugha yao ambayo kwa kawaida sarufi huwa na makosa. Matatizo hayo
yanasababisha mahitaji ya muda zaidi. Hivyo waraka huu unawapa
nyongeza ya muda wa dakika 20 kwa kila saa ya somo la Hisabati na
dakika 15 kwa kila saa ya masomo mengine ya mtihani.
Kutokana na utaratibu huu wenye ulemavu waandaliwe mkondo wao, wenye
wanafunzi pekee ili ratiba iweze kufuatwa kwa urahisi.
Aidha, kuhusu usimamizi, inaagizwa wanafunzi wenye ulemavu wasimamiwe
na mwalimu mtaalamu wa Elimu maalum kulingana na aina ya ulemavu
uliopo shuleni.
Wakati wa kusahihisha mitihani hii, walimu watalamu wa wanafunzi wenye
ulemavu wahusishwe ili kushauri katika kazi hiyo kuwezesha utekelezaji wa
masuala hayo, maelekezo yote toka Baraza la Mitihani la Tanzania yazingatie
maelekezo hayo ili kuwezesha utekelezaji fanisi wa waraka huu.
Waraka huu unaanza kutumika Mara moja
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
1. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
2. Wakurugenzi wote Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
33
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. ED/OKE/NYE/VOL.1/12
SANDUKU LA POSTA
9121
DAR ES SALAAM
Tarehe 29/04/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu
Wakuu wa Shule za Sekondari
Walimu Wakuu wa Shule za Awali/Msingi
TANZANIA BARA
WARAKA WA ELIMU NA. 12 WA MWAKA 2011
KUKARIRISHA DARASA KUHAMISHA AU KUFUKUZA WANAFUNZI WA
SHULE ZA SEKONDARI
Imebainika kwamba, kuna shule za sekondari hasa zisizo za serikali,ambazo
zinaendelea kukaririsha darasa, kuhamisha au kuwafukuza shule wanafunzi bila
kufuata utaratibu uliotolewa, hata baada ya kutolewa Waraka namba 2 wa
mwaka 1997 na Waraka namba 6 wa mwaka 2007.
Ninapenda kuwakumbusha kwamba, muundo wa elimu ya sekondari katika
Tanzania Bara ni miaka minne kwa elimu ya sekondari ya kawaida na miakamiwili ya elimu ya sekondari ya juu. Mwanafunzi anapochaguliwa kusoma katika
shule ya sekondari, anatakiwa asome kwa mfululizo kuanzia kidato cha kwanza
hadi cha nne na kuanzia kidato cha tano hadi cha sita.
Hayo ndiyo matarajio ya serikali, wazazi/walezi na wanafunzi wenyewe.
Umezuka mtindo wa baadhi ya Wakuu wa Shule zisizokuwa za serikali
kuwakaririsha wanafunzi, kuwahamisha au kuwafukuza shule kwa kisingizio
kwamba hawakufikia wastani wa shule.
Wizara inawakumbusha kwamba, kufanya hivyo ni kinyume cha matarajio ya
serikali wazazi/walezi na wanafunzi, kwani kunawaongezea mzigo wazazi,
34
kuwapotezea muda wanafunzi na kulifanya taifa lishindwe kufikia malengo yamilenia na malengo ya elimu kwa wote.
Kwa Waraka huu, ninaagiza kwamba kuanzia sasa hakuna shule
itakayoruhusiwa kukaririsha, kuhamisha au kufukuza mwanafunzi kwa sababu ya
kutokufikisha wastani uliowekwa na shule.
Ili kuhakikisha agizo hili linafanikiwa, kila shule itatakiwa kufanya yafuatayo
wakati wa kuandikisha wanafunzi wa Kidato cha Kwanza na cha Tano:
„h Kila tarehe 31 Machi ya kila mwaka, Mkuu wa shule atatakiwa aweamewasilisha orodha ya wanafunzi wote aliowaandikisha Kidato cha
Kwanza katika shule yake Baraza la Mitihani Tanzania, Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi na OWM-TAMISEMI
„h Kila tarehe 30 Aprili ya kila mwaka, Mkuu wa shule atatakiwa aweamewasilisha orodha ya wanafunzi wote aliowaandikisha Kidato cha
Tano katika shule yake Baraza la Mitihani Tanzania, Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi na OWM -TAMISEMI.
Orodha hizi zitakazowasilishwa zitatoa takwimu halisi za wanafunzi
walioandikishwa kwa mwaka husika na hata kama mwanafunzi atahamishwa
kwa sababu yoyote ile itajulikana ametoka shule gani na amekwenda shule gani.
Aidha, takwimu hizi zitalisaidia Baraza la Mitihani la Tanzania kuweza kupanga
mipango yake ya baadaye pamoja na kutambua shule zinazofanya vizuri kwa
kuweza kufaulisha wanafunzi kwa kulinganisha walioandikishwa na waliomaliza
(Completion Rate).
Taratibu nyingine za kukariri zitafuata maelekezo kama ifuatavyo:-
„h Mwanafunzi anayeomba na kukubaliwa kukariri katika ngazi yasekondari Kidato cha I - IV atapewa fursa ya kukariri mara moja.Endapo mamlaka inayohusika itaona umuhimu wa mwanafunzi
kukariri darasa ataweza kupewa fursa ya kukariri mara mbili.Hakuna mwanafunzi atakayeruhusiwa kukariri darasa zaidi ya mara
mbili katika ngazi hii. Kwa wale wanaosoma katika Kidato cha V na
VI watapewa fursa ya kukariri mara moja tu. Wizara inasisitiza
kwamba maombi yatakayokubaliwa ni yale ambayo kutokana na
sababu mbalimbali mwanafunzi amekosa masomo kwa siku 90 auzaidi mfululizo kwa kukosa ada au kuwa mgonjwa na ugonjwaukathibitishwa na daktari.
Uamuzi huu utatekelezwa kama ifuatavyo:
„h Waombaji wanaosoma Kidato cha I - II, III au V watatakiwakuandika barua za maombi ya kukariri darasa kwa Katibu Tawala
wa Mkoa kupitia kwa Mkuu wa Shule anakosoma.
35
„h Maombi, kwa wale wanaotaka kukariri kidato cha IV au VI
yapelekwe kwa Kamishna wa Elimu kupitia kwa Mkuu wa Shulewanakosoma wanafunzi.
„h Kila barua ya maombi ni lazima iwe na viambatisho vifuatavyo:
„h Picha 2 “passport size”
„h Nakala ya fomu ya maendeleo ya mwanafunzi.
„h Uthibitisho wa sababu ya kukariri, kwa mfano: -a) Nakala ya vyeti vya matibabu na barua ya daktari alikotibiwa
mwanafunzi
b) Fomu namba 3 ya polisi (PF3) au barua ya Mahakama kwa
maswala ya jinai
c) Nakala ya barua ya uhamisho wa mzazi/mlezi.
d) Nakala ya barua toka kwa mzazi/mlezi kuwa mwanafunzi
amekosa ada
Waraka huu unasisitiza utekelezaji wa Waraka Na. 6 wa Mwaka 2007, nautaanza kutumika tarehe 1 Januari mwaka 2012. M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
„h Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania
„h Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI
„h Wakurugenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
„h Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kandana Wilaya.
36
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. ED/OKE/NYE/VOL.1/14
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 28/04/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
Maafisa Elimu wa Msingi/Sekondari wa Wilaya
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu
Wakuu wa Shule za Sekondari
Walimu Wakuu wa Shule za Awali/Msingi
TANZANIA BARA
MWONGOZO WA UVAAJI WA SARE ZA SHULE NA MWONEKANO
NADHIFU WA WANAFUNZI/WANACHUO
Kumejitokeza ukiukwaji wa sheria na kanuni za uendeshaji wa shule/vyuo
hususan katika uvaaji wa sare za shule na usafi wa mwili. Baadhi ya wanafunzi
wamekuwa wakivaa sare zinazokiuka taratibu za shule, mfano, kuvaa nguo za
kubana na fupi kwa wasichana na milegezo kwa wavulana. Aidha, baadhi ya
wanafunzi wanafuga na kupaka rangi kucha, wanafuga ndevu, kuwa na nywele
ndefu pamoja na mapambo mbalimbali.
Kutokana na kukithiri kwa hali hiyo katika baadhi ya shule, Wizara imelazimika
kuwakumbusha walimu wakuu wa shule za msingi, wakuu wa shule za sekondari
na vyuo vya Ualimu kuzingatia na kusimamia sheria na kanuni za uendeshaji wa
shule/vyuo zilizopo ili kulinda maadili na nidhamu shuleni/vyuoni.
Kwa waraka huu, inaagizwa kuwa mwanafunzi anatakiwa kuvaa sare ya shule
ipasavyo, na awe nadhifu kwa kuwa na nywele fupi, kukata kucha, kutopaka
rangi kucha, na kunyoa ndevu. Aidha, wasichana wawe na nywele fupi au
kusuka nywele za mistari kwenda nyuma.
Mwongozo huu usomwe sambamba na mwongozo kuhusu uvaaji wa hijab na
sala ya Ijumaa uliotolewa tarehe 18/08/1999.
37
Mwongozo huu, unaanza kutumika mara moja
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
1. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
2. Wakurugenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
38
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na ED/OKE/NYE/VOL.1/15
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 28/04/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
Maafisa Elimu Msingi/Sekondari wa Wilaya
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu
Wakuu wa Shule za Sekondari
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi
TANZANIA BARA
MWONGOZO WA UJAZAJI WA ALAMA ZA MITIHANI YA WANAFUNZI
KATIKA SEL FORMS NA TSM 9
Sel forms kwa wanafunzi wa sekondari na TSM 9 kwa wanafunzi wa shule zamsingi ni muhimu sana kwa sababu zinaonesha taarifa za maendeleo ya
mwanafunzi kitaaluma na kitabia. Taarifa zinazojazwa katika fomu hizi
zinatokana na alama za majaribio na mitihani ya mwisho wa mihula.
Pamekuwepo na ukiukwaji wa taratibu za ujazaji wa alama katika sel forms naTSM 9 kwa kujaza alama za kughushi. Hali hii husababisha kukosekana kwa
uwiano kati ya alama za maendeleo ya baadhi ya wanafunzi na matokeo yao ya
mitihani ya kitaifa.
Wizara inaagiza kuwa wakuu wa shule, walimu wakuu na walimu wote nchini
kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu na miongozo ya upatikanaji wa alama za
maendeleo ya kila siku ya mwanafunzi na kuzijaza ipasavyo kwenye fomu
husika.
Mwongozo huu unawakumbusha walimu wote kuzingatia maelezo
yaliyotolewa na unaanza kutumika mara moja.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
39
Nakala:
1. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
2. Wakurugenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
40
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb.Na. ED/OKE/193/292/02/86
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 06/05/2011
Wakuu wa Shule za Sekondari
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi
TANZANIA BARA
YAH: USIMAMIZI WA SHUGHULI ZOTE ZA SHULE
Wizara inatambua kazi nzito mliyonayo ya kusimamia shughuli za shule nchini.
Hata hivyo, imeona ni vyema kukumbushana katika baadhi ya maeneo.
Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya walimu wakuu wa shule kutokuwepo katika
maeneo yao ya kazi kwa muda mrefu kwa kisingizio cha kuhudhuria semina na
mafunzo elekezi na kuacha shule ikiendeshwa na walimu wasaidizi au walimu
wa kawaida. Hali hii inasababisha kutokuwepo na usimamizi madhubuti wa
shule, na baadhi ya walimu kupata mwanya wa kutoingia madarasani na
kutofundisha wanafunzi ipasavyo.
Kwa barua hii wakuu wa shule, walimu wakuu wanatakiwa
„h Kuwepo shuleni siku zote 194.
„h Kuangalia ufundishaji wa walimu wakuu na ujifunzaji wanafunzi ili kuepushamanung’uniko ya wazazi/walezi.
„h Kuhakikisha kwamba walimu wote wanafundisha ipasavyo kutokana namadaraka waliyopewa.
Kama kutakuwepo na mafunzo elekezi, semina au vikao, ni vema shughuli hizo
zikaendeshwa wakati wa likizo fupi na ndefu au wakati wa mwisho wa wiki. Hiiitawezesha wakuu wa shule, walimu wakuu kufanya kazi ya usimamizi wa shule
ipasavyo kutokana na madaraka waliyopewa.
Kwa yeyote atakayekiuka na kutofuata maazigo ya barua hii atachuliwa hatua za
kinidhamu.
41
Nakutakia kazi njema.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
1. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
2. Wakurugenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
3. Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
4. Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
5. Wakurugenzi; Halmashauri za Miji/Manispaa/Jiji
6. Wakurugenzi Watendaji; Halmashauri za Wilaya
7. Maafisa Elimu wa Mikoa
8. Maafisa Elimu wa Wilaya (Msingi/Sekondari)
9. Katibu Mkuu wa TAHOSSA10.Katibu Mkuu, TAMONGSCO
42
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb.Na. ED/OKE/C.5/03/78
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 14/07/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi wakuu wa shule wa Wilaya
Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji Manispaa na Jiji
Wakuu wa Shule za Sekondari
TANZANIA BARA
YAH: KIBALI CHA KUFANYA MTIHANI WA DINI YA KIISLAM KWAWANAFUNZI WA DARASA LA SABA
Wizara ilipokea maombi kutoka “Islamic Education Panel’ kutaka kuwepo kwa
mtihani wa Dini wa Kitaifa kwa wanafunzi wa darasa la Saba.
Kwa kutambua umuhimu wa Somo la Dini kwa wanafunzi wetu Wizara imetoa
kibali Mtihani wa Dini ya Kiislamu kwa wanafunzi wanaohitimu Darasa la Saba
uanze kufanyika mwaka 2011.
Kwa mwaka 2011 mtihani huo utafanyika siku ya Jumatano, tarehe 10/8/2011.
Aidha, kila mwaka tarehe muafaka itakayofanyika siku ya Jumatano kila mwezi
Agosti itateuliwa. Mtihani huo utaendeshwa kwa gharama za “Ilamic Education
Panel”.
M.M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
1. Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
2. Wakurugenzi wote, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
43
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. OKE/NYE/VOL.I/19
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 16/12/2011
Makatibu Tawala wa Mkoa,
Makatibu Tawala wa Wilaya,
Wakurugenzi; Halmashauri za Miji/Manispaa/Jiji,
Wakurugenzi Watendaji; Halmashauri za Wilaya,
Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya,
Wakuu wa Shule za Sekondari,
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi.
TANZANIA BARA.
WARAKA WA ELIMU NA. 14 WA MWAKA 2011
WANAFUNZI WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA WANAOCHAGULIWA
KUINGIA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
KUTOPOKELEWA.
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 imeainisha malengo ya Elimu ya
Msingi. Mojawapo ya malengo haya ni kumwezesha mwanafunzi kujifunza stadi
za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.
Katika miaka ya hivi karibuni kumeibuka tatizo la kuwepo kwa wanafunzi
wasiojua Kusoma na Kuandika katika baadhi ya shule za sekondari. Hali hii
imeibua hisia nyingi miongoni mwa wadau wa elimu ikiwa ni pamoja na
kulalamikia umuhimu wa kuwepo kwa Mtihani wa Darasa la Nne na Kidato cha
Pili. Mitihani hiyo ni ya muhimu sana kwa wanafunzi kwani itaweza kuwachuja na
kupata wanafunzi wazuri na kuweka misingi bora ya wanafunzi katika ujifunzaji.
Ili kurekebisha dosari hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaagiza wakuu
wa shule za Sekondari kutowapokea wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika
44
kujiunga na Elimu ya Sekondari. Aidha, wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga
na elimu ya sekondari kila mwaka wafanyiwe jaribio la kupima stadi za kusoma,
kuandika na kuhesabu katika ngazi ya shule ya sekondari kabla ya kuanza
masomo yao rasmi. Zoezi hili lifanywe na wakuu wa shule katika shule ya
sekondari mwanafunzi alipochaguliwa. Zoezi hili ni la muhimu na lifanywe kwa
umakini ili kupata wanafunzi wenye sifa stahiki kuendelea na masomo ya
sekondari. Jaribio hili lisiwe na gharama zozote toka kwa wazazi hasa michango
ya fedha.
Mwanafunzi atakayeshindwa jaribio hilo hataruhusiwa kuanza masomo ya Elimu
ya Sekondari na endapo itagundulika kuwepo na udanganyifu katika Mtihani wa
kuhitimu Darasa la Saba ambao amefanya mwanafunzi husika, hatua za
kinidhamu zitachukuliwa kwa waliohusika na udanganyifu huo.
Waraka huu unaanza kutumika tarehe 1 Januari,2012.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala: Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.
Mkurugenzi, Taasisi ya Elimu Tanzania.
Wakurugenzi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
45
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Cable: ELIMU DAR ES SALAAM.
PHONE: 2123686
Telex: 242741 Elimu Tz.
Email: escc@intafrica.com
Webaite:www.moe.go.tz
Reply please quote:
Kumb. Na. EB/OK/C.2/4/49
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 28/12/2011
Makatibu Tawala wa Mikoa,
Wakurugenzi; Halmashauri za Miji/Manispaa/Jiji,
Wakurugenzi Watendaji; Halmashauri za Wilaya,
Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya,
Mameneja na wenye Shule,
Wakuu wa Shule za Sekondari
TANZANIA BARA
WARAKA WA ELIMU NA. 16 WA MWAKA 2011
WASTANI WA UFAULU KATIKA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA PILI
Mtihani wa taifa Kidato cha Pili ulianzishwa mwaka 1984 kwa madhumuni ya
kupima maendeleo ya wanafunzi baada ya miaka miwili ya Elimu ya Sekondari.
Mtihani huu ni tathmini ya kati inayopima kiwango cha maarifa na ujuzi aliopata
mwanafunzi kutokana na masomo aliyojifunza katika Kidato cha Kwanza na cha
Pili. Aidha, unalenga kuwapatia motisha walimu na wanafunzi ili waongeze bidii
na kuinua viwango vya maendeleo ya wanafunzi kitaaluma.
Shabaha ya serikali ni kutoa elimu katika ngazi zote ikiwemo ya sekondari kwa
kuwafanya walimu na wanafunzi wawajibike ipasavyo. Mtihani wa Kidato cha Pili
ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa wazazi, walimu na wanafunzi
wanawajibika ipasavyo.
Utafiti uliofanyika mwaka 2011 ulibainisha sababu mojawapo ya wanafunzi
kufanya vibaya ni kutokana na kuwaruhusu kuendelea na masomo hata baada
ya kushindwa kufikia alama ya ufaulu katika mtihani wa Kidato cha Pili. Aidha,
wanafunzi, wazazi, walimu na wadau wengine walionesha haja ya ufaulu wa
mtihani wa Kidato cha Pili kuwa kipimo cha kuendelea na masomo ya Kidato cha
Tatu.
46
Baadhi ya shule za sekondari zisizokuwa za serikali zimekuwa na alama tofauti
za ufaulu wa mtihani huo na kuwanyima fursa baadhi ya wanafunzi ya kuendelea
na masomo ya Kidato cha Tatu katika shule zao kwa alama za ufaulu
walizojiwekea.
Kwa mantiki hiyo, Wizara inaendelea kusisitiza kuwa kiwango cha alama ya
ufaulu ni 30%. Kiwango hiki ni kwa shule za serikali na zisizo za serikali.
Mwanafunzi ambaye atashindwa kupata alama hizo atalazimika kukariri kidato
cha pili mara moja tu na iwapo atashindwa kufikia alama ya ufaulu ataondolewa
katika mfumo rasmi wa elimu.
Waraka huu unarekebisha Waraka Na. 5 wa Mwaka 2008 na unaanza kutumika
Januari, 2012.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
„h Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI
„h Mkurugenzi, Taasisi ya Elimu Tanzania,
„h Wakurugenzi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
47
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. ED/OKE/NE/VOL.1/01/8
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 10/01/2012
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda,
Maafisaelimu Mikoa,
Maafisaelimu Wilaya (Sekondari),
Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali,
YAH: MWONGOZO WA UTEKELEZAJI WA WARAKA WA ELIMU NA. 14 WAMWAKA 2011 WA NAMNA YA KUTAHINI STADI ZA KUSOMA NA
KUANDIKA KWA WANAFUNZI WANAOJIUNGA NA KIDATO CHA
KWANZA
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatoa mwongozo huu ili kuwa na
ulinganifu mzuri wa kutahini stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu kwa
wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari kuanzia mwaka 2012 kwa nchi
nzima. Wanafunzi wa chaguo la kwanza wapimwe mwezi Februari, na wale wa
chaguo la pili wapimwe mwezi Aprili kila mwaka.
Ili zoezi hili lifanyike kwa ufanisi itabidi mwanafunzi atahiniwe kwa utaratibu
akianza na kusoma, kuandika na hatua ya mwisho kuhesabu kwa kufanya
mojawapo ya yafuatayo:
Stadi Mazoezi Aendelee
Kusoma Kusoma kifungu (para) ya
hadithi kwa sauti (maneno 25)
Kusoma maneno
yasiyopungua 20 kama
inavyotakiwa
Kuandika imla (maneno 25) Aandike maneno
yasiyopungua 20 kama
inavyotakiwa
Kuandika
Kuandika hadithi fupi au barua
fupi
Aandike maneno vizuri
yanayosomeka na
kuleta maana
Kusoma na
Kuandika
Kusoma kifungu (para) cha
hadithi isiyo na misamiati
migumu na kujibu maswali 5
yaliyo wazi
Ajibu maswali 3
yanayohusu hadithi
hiyo kwa usahihi
48
Kuhesabu Hesabu 10 rahisi za
kujumlisha, kutoa, kuzidisha na
kugawa
Afanye hesabu 8 kwa
usahihi
Kuhesabu na
kuandika
Apewe picha za maumbo 5
(duara, mstatili, pembetatu,
mstari, miraba)
Aandike majina ya
maumbo hayo kama
inavyotakiwa
Mkuu wa shule akishirikiana na walimu atayarishe mazoezi hayo kwa lugha ya
Kiswahili na Kingereza ili mwanafunzi atahiniwe kwa lugha aliyotumia katika
elimu ya msingi.
Aidha, zoezi hili lihusishe walimu wote katika shule ili líweze kukamilika ndani ya
siku moja. Majina ya watahiniwa watakaoshindwa yawasilishwe kwa Afisaelimu
Mkoa.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
49
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Kumb. Na. CHA-281/478/01/56 Tarehe: 01/02/2012Makatibu Tawala wa Mkoa,
Makatibu Tawala wa Wilaya,
Wakurugenzi; Halmashauri za Miji/Manispaa/Jiji,
Wakurugenzi Watendaji; Halmashauri za Wilaya,
Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya,
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu,
Wakuu wa Shule za Sekondari,
TANZANIA BARA
WARAKA WA ELIMU NA. 1 WA MWAKA 2012
KUREJESHWA KWA ADA YA MTIHANI KWA SHULE ZA SEKONDARI ZA
SERIKALI
Uendeshaji wa Mitihani ya Taifa una shughuli mbalimbali zinazohitaji fedha
nyingi. Kwa miaka yote, Serikali huchukua sehemu kubwa ya gharama za
kuendesha mitihani ya kitaifa ikiwa ni pamoja na gharama za utunzi, uchapaji,
usambazaji, usimamizi, usahihishaji na uchambuzi wa matokeo. Sehemu
nyingine ya gharama hizi inachangiwa na watahiniwa wenyewe.
Mwaka 2009, Serikali ilisitisha uchangiaji katika mitihani ya Kitaifa kwa wanafunzi
wote wa shule za Serikali wanaofanya mitihani ya Kidato cha 2, Kidato cha 4 na
Kidato cha 6. Watahiniwa wa kujitegemea (Private Candidates) na wa shule
binafsi ambao ni asilimia ndogo ya watahiniwa ndio walioendelea kuchangia
gharama za mitihani.
50
Kwa kuwa gharama za uendeshaji wa mitihani zimeendelea kuwa kubwa mwaka
hadi mwaka, Serikali imeamua kurudisha ada za Mitihani kwa shule za Serikali ili
kuchangia gharama. Watahiniwa watalipa Ada za mitihani kama ifuatavyo:-
Mtihani wa Kidato cha 2 sh. 10,000/= kila Mtahiniwa
Mtihani wa Kidato cha 4 sh. 35,000/= kila Mtahiniwa
Mtihani wa Kidato cha 6 sh. 35,000/= kila Mtahiniwa
Ada hizi zitalipwa na wanafunzi wote wa shule za Serikali, shule zisizo za serikali
na watahiniwa wa kujitegemea. Ada hizi zitaanza kulipwa kwa mitihani yote ya
kitaifa (Kidato cha 2, 4, 6) itakayoanza mwaka 2012/13.
Baraza la Mitihani litatoa maelekezo zaidi kuhusu tarehe za kufanya malipo
hayo.
Kwa kuwa michango ya watahiniwa ni sehemu tu ya gharama stahili, Serikali
itaendelea kuchukua sehemu kubwa ya gharama za uendeshaji wa mitihani ya
Kitaifa.
Waraka huu unaanza kutumika mwaka wa fedha 2012/13 na unafuta waraka Na
1 wa mwaka 2010.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala : Katibu Mkuu Kiongozi,Ofisi ya Rais, Ikulu
S. L. P. 9120
DAR ES SALAAM
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais,
Idara Kuu ya Utumishi wa Umma,
S. L. P. 2483
DAR ES SALAAM
Katibu Mkuu,
OWM - TAMISEMI,
S. L. P. 1923,
DODOMA
51
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. ED/OKE/NYE/VOL. 1/15
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 06/02/2012
Makatibu Tawala wa Mkoa,
Makatibu Tawala wa Wilaya,
Wakurugenzi; Halmashauri za Miji/Manispaa/Jiji,
Wakurugenzi Watendaji; Halmashauri za Wilaya,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya,
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu,
Wakuu wa Shule za Sekondari,
Waratibu Elimu Kata,
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi.
WARAKA WA ELIMU NA. 2 WA MWAKA 2012
UMUHIMU WA WALIMU KUHUDHURIA VIPINDI DARASANI NA
KUFUNDISHA
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatambua wajibu wa walimu katika
kutekeleza azma ya Serikali ya kulipatia Taifa huduma ya Elimu nchini. Aidha,
wizara inaheshimu jitihada na uvumilivu unaonyeshwa na walimu katika
kutekeleza azma hii ya serikali pamoja na kwamba mara nyingi elimu inatolewa
katika mazingira magumu. Wizara inawapongeza wale wote wanaotekeleza
wajibu wao kwa moyo wa kujituma na wa kizalendo.
Pamoja na jitihada zinazoonyeshwa na walimu wengi, wapo walimu wachache
ambao wana tabia ya kuondoka shuleni na kuacha wanafunzi bila msaada
wowote wa kujifunza kwa visingizio kuwa wanafuatilia shida zao katika ofisi za
elimu Mkoani au Wilayani/Halmashauri. Aidha, baadhi ya walimu huondoka
shuleni na kuwatelekeza wanafunzi kwa madai kwamba wanakwenda
kuhudhuria mikutano ambayo haina uhusiano au haichangii kuboresha utoaji wa
elimu.
52
Hali hii inalelewa na baadhi ya walimu wakuu, wakuu wa shule na wakuu wa
vyuo vya ualimu ambao wanaona utovu huu wa nidhamu ukiendelea bila
kuchukua hatua zinazostahili kukomesha tabia hiyo. Tabia nyingine ni ile ya
kuwaacha wanafunzi bila kufundishwa licha ya mwalimu kuwepo shuleni. Tabia
hii inakiuka maadili ya ualimu na kuvunja sheria na kanuni za utumishi.
Kutokana na hali hii, Wizara inaagiza kuwa mwalimu yeyote ambaye
hatafundisha vipindi vyake bila sababu za msingi atachukuliwa hatua za kisheria
ikiwa ni pamoja na kukatwa mshahara wake kwa kipindi chote ambacho
hakuhudhuria vipindi na kufundisha. Aidha, mwalimu mkuu, mkuu wa shule/chuo
cha ualimu ahakikishe kuwa walimu wanahudhuria vipindi na kufundisha
wanafunzi ipasavyo ili kuleta ufanisi.
Ripoti ya mwalimu atakayeshindwa kutimiza wajibu wake ipelekwe mara moja
kwa Mkurugenzi wa Wilaya/Halmashauri husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua
za kinidhamu.
Waraka huu unawakumbusha walimu kuwa ni watumishi wa serikali ambao
wameajiriwa chini ya sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa serikali na
utumishi wa walimu (TSD), hivyo wanapaswa kufuata na kuzingatia sheria na
kanuni hizo katika ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi darasani.
Ni matumaini ya wizara kuwa walimu wakuu, wakuu wa shule/vyuo vya ualimu
watatoa ushirikiano unaostahili kwa walimu ili kuboresha elimu nchini.
Waraka huu unarekebisha Waraka wa Elimu Na. 14 wa mwaka 1997 na utaanza
kutumika mwaka 2012.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala: Katibu Mkuu OWM – TAMISEMI.
53
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. ED/OKE/NYE/VOL.I/18
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 21/05/2012
Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu
Wakuu wa Shule za Sekondari
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi
TANZANIA BARA.
WARAKA WA ELIMU NA 3 WA MWAKA 2012
WANAFUNZI KUFUKUZWA SHULE/CHUO KABLA YA MTIHANI WA TAIFA
KUFANYIKA
Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 na Rekebisho lake Sura ya 353 Kifungu Na.
35(3) ya mwaka 2002, inaeleza kuwa kila mwanafunzi akijiandikisha shule hana
budi kuhudhuria na kumaliza shule katika ngazi husika. Aidha, mipango yote ya
Elimu: Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi [MMEM] na Mpango wa
Maendeleo ya Elimu ya Sekondari [MMES], inasisitiza wanafunzi kuandikishwa,
kuhudhuria na kumaliza masomo yao katika ngazi husika.
Pamoja na kwamba ni lazima wanafunzi walioandikishwa kuhudhuria na
kumaliza masomo katika ngazi husika ya elimu, baadhi ya shule/vyuo
wamekuwa na utamaduni wa kuwasimamisha au kuwafukuza shule/chuo
wanafunzi wakati mitihani inapokaribia kutokana na makosa mbalimbali ya utovu
wa nidhamu. Kamati au Bodi za Shule/Chuo hutoa adhabu ya kuwafukuza
wanafunzi hao shule/chuo wakati wanakaribia kufanya mitihani yao ya mwisho
kwa ajili ya kuhitimu ngazi husika ya masomo.
Matatizo mengi ya utovu wa nidhamu yangeweza kushughulikiwa mapema na
shule au chuo badala ya kusubiri wakati mitihani inapokaribia. Kitendo cha
54
kufukuza wanafunzi wakati mitihani inapokaribia kinasababisha usumbufu
mkubwa kwa wanafunzi wenyewe na wazazi/walezi wao. Vilevile, hali hiyo
inaisababishia Serikali hasara kubwa ya gharama ya maandalizi yote ya mitihani
ya Taifa.
Kutokana na hali hiyo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaagiza kuwa
mwanafunzi/mwanachuo yeyote asipewe adhabu ya kufukuzwa shule/chuo
miezi mitatu kabla ya mitihani ya Taifa ya kuhitimu ngazi husika ya elimu.Badala yake adhabu mbadala itolewe kwa wanafunzi ili kuondoa usumbufu kwa
wanafunzi wenyewe na wazazi au walezi wao. Endapo Kamati au Bodi
italazimika kumsimamisha masomo mwanafunzi wakati au ndani ya kipindi cha
mitihani, mwanafunzi huyo asinyimwe kufanya mitihani na badala yake
aruhusiwe kufanya mitihani hiyo katika kituo chake akiwa nje ya utaratibu wa
shule.
Ni jukumu la uongozi wa shule na walimu wote kujua mienendo na tabia za
wanafunzi mapema ili kuepusha tatizo la kuwafukuza shule/chuo muda mfupi
kabla ya mtihani wa kitaifa kufanyika.
Waraka huu unarekebisha mwongozo uliotolewa tarehe 28/03/2011 pamoja na
Waraka wa Elimu wa tarehe 09/12/2011 kuhusu wanafunzi kufukuzwa
shule/chuo inapokaribia mitihani ya taifa kufanyika.
Waraka huu unaanza kutumika mara moja.
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
„h Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI
„h Wakurugenzi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.