WELL COME ULIMAKAFU SCHOOL WEB SITE.
KARIBUNI ULIMAKAFU SHULE YA MSINGI
Ulimakafu shule ya msingi ni moja ya shule zilizopo mkoa wa Tabora.wilaya ya Tabora vijijini kata ya Ilolangulu Tarafa ya Ilolalangulu Kijiji cha ulimakafu .Katika kijiji hiki kunashule mbili ambazo ni Kagobole na Ulimakafu.Sulehii inawanafunzi 350 ina walimu 12 wakike 7 wakiume 5
Shule hii imefanikiwa kufanya vizuri katika shule za wilaya ya Tabora vijijini na imeshika nafasi ya kwanza kwa miaka mitatu mfululizo.Hii ni juhudi za walimu na wanafunzi.
HOTUBA FUPI YA MWALIMU PAUL MEELA KUHUSU MFUMO WA ELIMU.
Ndugu zangu watanzania,
“Mfumo wa elimu ya
Matatizo ya elimu Nchini
Lengo kubwa la elimu ni kumuandaa mtu ili aweze kukabiliana na mazingira yanayomzunguka.Si lengo la elimu mtu kuzunguka na vyeti kutafuta kazi za ofisini tu.Katika fikra za MWALIMU alisema elimu ya Tanzania ni lazima imuandae mtanzania ili aweze kujitegemea mwenyewe ikiwa ni pamoja uwezo wa kuwa na fikra sahihi pamoja maamuzi sahihi(mambo sahihi hutokana na fikra sahihi)
-Asilimia kubwa ya walimu wa Tanzania wamekuwa walimu baada kukosa nafasi kwenye taaluma nyingine.
-Wanafunzi wengi wa shule za msingi wanakaa chini na wengine chini ya miti.
-Walimu wachache waliopo hawana maslahi ya kutosha hivyo wamekata tamaa.
-Asilimia kubwa ya walimu ni wale waliofaulu viwango wa chini sana kwenye elimu ya sekondari.
-Idadi kubwa ya wanafunzi darasani kuliko uwezo wa darasa.
-Shule kukosa nyumba za walimu.
-Kutokuwa na bodi ya walimu.
-Mtihani shule za msingi kuwa na maswali ya kuchagua tu(multiple choice) mpake hesabu.
KWA KUZINGATIA NILIYOYATAJA,LENGO LA ELIMU TANZANIA LINAFIKIWA?
1GOAL Tanzania: Elimu kwa wote
Aliyeko katika picha hapa juu ni Mwalimu Mkuu Ndugu PAUL MEELA